Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kinashiriki katika Wiki ya Maadhimisho Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu kwa kuonyesha bunifu zalishi nane zinazolenga kutoa suluhisho kwa changamoto katika afya, kilimo na ustawi wa jamii.

Bunifu hizo ni pamoja na ROBOSPINE, inayosaidia watoto wenye spina bifida kusimama, kutembea na kufanya mazoezi; BILIMEASURE, inayopima kiwango cha bilirubin kwa watoto wachanga bila kuchukua damu; na SIKUSMART, inayotabiri mzunguko wa hedhi na kipindi cha yai kupevuka bila simu janja au intaneti.
Nyingine ni BRIDGING SILENCE, inayotumia Akili Bandia (AI) kutafsiri lugha ya alama kuwa maandishi na sauti ya Kiswahili; BIOSAFE, kiuatilifu hai cha asili kinachosaidia kudhibiti magonjwa ya mimea; MoyoGuard, inayorekodi mapigo ya moyo ndani ya sekunde 30 bila intaneti; na QR DHARURA, inayorahisisha upatikanaji wa taarifa muhimu za mtu wakati wa dharura.

Kupitia bunifu hizi, MUHAS inaendelea kugeuza elimu, utafiti na teknolojia kuwa suluhisho bunifu zenye manufaa kwa jamii, huku ikichangia kuboresha afya, kukuza ujumuishi, kulinda mazingira na kuongeza ustawi wa wananchi.

