Na Muhidin Amri Namtumbo

WAKATI Serikali kupitia Bodi ya Tumbaku Tanzania imetangaza kuongeza bei elekezi ya zao la tumbaku kwa msimu wa kilimo wa 2026/2027 kutoka dola za Marekani 1.95 kwa kilo katika msimu uliopita hadi dola 2.05 kwa kilo ili kuwapa motisha wakulima kuongeza uzalishaji na kuinua tija ya zao hilo.

Mbunge wa Jimbo la Namtumbo ambaye pia ni Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Juma Zuberi Homera, amewataka wakulima katika jimbo hilo kutokata tamaa na kuendelea kulima mazao ya tumbaku na mahindi licha ya changamoto zinazojitokeza katika masoko na kushuka kwa bei ya baadhi ya mazao hayo.

Dkt. Homera ametoa rai hiyo akiwataka wakulima wa tumbaku kuwa na subira wakati Serikali ikiendelea kuchukua hatua za kukabiliana na changamoto za soko na kuhakikisha zao hilo linapata bei inayomnufaisha mkulima.

“Tuvumilie kidogo tukiwa tunaendelea kupambana na hawa watu, Serikali ya Awamu ya Sita itapambania hilo na bei itakuwa nzuri,” amesema Dkt. Homera.

Amesema Serikali inaendelea kufuatilia kwa karibu changamoto zinazowakabili wakulima, akisisitiza kuwa lengo ni kuhakikisha wananchi wanaonufaika na kilimo hawapati hasara kutokana na changamoto za masoko au kuingiliwa na walanguzi.

Kwa upande wa zao la mahindi, Dkt. Homera amewataka wakulima kutouza mazao yao yote kwa haraka, bali kuwa na subira huku Serikali ikiendelea kutafuta masoko ya uhakika yatakayowawezesha kupata thamani stahiki ya jasho lao.

Amesema Serikali ipo kwa ajili ya kuwalinda na kuwawezesha wakulima, ikiwemo kuwatafutia masoko ya uhakika ili kuondokana na hali ya wakulima kulazimika kuuza mazao yao kwa bei ndogo kwa walanguzi.

Katika hatua nyingine, Dkt. Homera amewahakikishia wakulima wa Namtumbo kuwa mbolea ya ruzuku aina ya DAP inatarajiwa kufika ndani ya siku saba, huku akieleza kuwa mbolea aina ya UREA inatarajiwa kuwasili tarehe 15 Septemba 2026.

Amesema mbolea hiyo ni sehemu ya mpango wa Serikali wa ruzuku kwa wakulima na itaanza kutolewa kupitia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) katika Wilaya ya Na

MBUNGE wa Jimbo la Namtumbo ambaye pia ni Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Juma Zuberi Homera, amewataka wakulima katika jimbo hilo kutokata tamaa na kuendelea kulima mazao ya tumbaku na mahindi licha ya changamoto zinazojitokeza katika masoko na kushuka kwa bei ya baadhi ya mazao hayo.

Dkt. Homera ametoa rai hiyo akiwataka wakulima wa tumbaku kuwa na subira wakati Serikali ikiendelea kuchukua hatua za kukabiliana na changamoto za soko na kuhakikisha zao hilo linapata bei inayomnufaisha mkulima.

“Tuvumilie kidogo tukiwa tunaendelea kupambana na hawa watu, Serikali ya Awamu ya Sita itapambania hilo na bei itakuwa nzuri,” amesema Dkt. Homera.

Amesema Serikali inaendelea kufuatilia kwa karibu changamoto zinazowakabili wakulima, akisisitiza kuwa lengo ni kuhakikisha wananchi wanaonufaika na kilimo hawapati hasara kutokana na changamoto za masoko au kuingiliwa na walanguzi.

Kwa upande wa zao la mahindi, Dkt. Homera amewataka wakulima kutouza mazao yao yote kwa haraka, bali kuwa na subira huku Serikali ikiendelea kutafuta masoko ya uhakika yatakayowawezesha kupata thamani stahiki ya jasho lao.

Amesema Serikali ipo kwa ajili ya kuwalinda na kuwawezesha wakulima, ikiwemo kuwatafutia masoko ya uhakika ili kuondokana na hali ya wakulima kulazimika kuuza mazao yao kwa bei ndogo kwa walanguzi.

Katika hatua nyingine, Dkt. Homera amewahakikishia wakulima wa Namtumbo kuwa mbolea ya ruzuku aina ya DAP inatarajiwa kufika ndani ya siku saba, huku akieleza kuwa mbolea aina ya UREA inatarajiwa kuwasili tarehe 15 Septemba 2026.

Amesema mbolea hiyo ni sehemu ya mpango wa Serikali wa ruzuku kwa wakulima na itaanza kutolewa kupitia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) katika Wilaya ya Namtumbo.

Amehimiza wananchi kutumia fursa hiyo kwa kuhakikisha wanapata mbolea hiyo ya ruzuku na kuitumia katika shughuli zao za kilimo ili kuongeza uzalishaji na tija.

Amesema ushirikiano kati ya Serikali na wakulima ni muhimu katika kukabiliana na changamoto za uzalishaji na masoko, huku akitoa wito kwa wananchi kuendelea kujikita katika kilimo na kutumia ipasavyo fursa zinazotolewa na Serikali.