Waziri wa katiba na sheria ambye ni Mbunge wa Jimbo la Namtumbo Mkoani Ruvuma Dkt Juma Zuber Homera kulia,akizungumza na baadhi ya wananchi wa kijiji cha Mlilayoyo Halmashauri ya wilaya Namtumbo aliowakuta kwenye ujenzi wa mradi wa shule  mpya ya Sekondari Mlilayoy

………

Na Mwandishi wetu, Namtumbo

MBUNGE wa jimbo la Namtumbo Dkt Juma Homera,amewataka wananchi kujitolea na kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa miradi ya mendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao.

Amesisitiza kuwa,ushiriki wa wananchi ni sehemu muhimu ya kuharakisha maendeleo na kuboresha huduma katika jamii.

Dkt Homera amesema hayo jana wakati akizindua ujenzi wa shule mpya ya sekondari ya Mlilayoyo  kaya ya Hanga inayojengwa kwa gharama ya Sh.milioni 560.

Akizungumza na wananchi waliokuwa katika eneo la mradi huo Dkt Homera alisema,maendeleo ya jamii hayawezi kuachwa kuwa jukumu ya serikali pekee,bali yanahitaji ushirikiano wa karibu wa wananchi kupitia nguvu zao.

“ukishiriki kwenye miradi ya maendeleo,wewe ni ni mzalendo wa kweli katika nchi yako,nawaomba wananchi wenzetu tuhakikishe tunashiriki kwa karibu kwenye ujenzi wa miradi inayotekelezwa katika maeneo yetu ili kuharakisha uchumi na kuboresha huduma za kijamii”alisema Dkt Homera.

Alisema,wananchi wanapojitokeza kushiriki katika ujenzi wa miradi ya maendeleo,wanaonyesha kwa vitendo kuwa wanaunga mkono juhudi za Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kuboresha huduma za kijamii na kuleta maendeleo ya wananchi.

Homera ambaye pia ni Waziri wa Katiba na sheria alisema,iwapo wananchi wataendelea kujitolea na kushiriki katika shughuli mbalimbali za ujenzi,wataweza kuisaidia Serikali kupunguza gharama za miradi inayotekelezwa na kuokoa fedha  ambazo zinaweza kutumika miradi mingine ya mendeleo.

Kwa mujibu wa Dkt Homera,ushiriki wa wananchi unapaswa kuonekana kama sehemu ya umiliki wa miradi inayotekelezwa katika maeneo yao kwani wanaposhiriki katika ujenzi huo huwa na uwezekano mkubwa wa kuilinda na kuhakikisha inatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.

Msimamizi wa ujenzi wa mradi huo mwalimu Athuman Kaniki alisema,fedha hizo zitatumika kujenga majengo ya utawala,vyumba vya madarasa 4 vyenye ofisi 2,vyumba vine vya madarasa visivyo na ofisi,maabara ya fizikia na bailojia,jengo la maktaba,Tehama na vyoo vya wanafunzi.

“Kwa sasa tunaendelea kukamilisha uchimbaji wa msingi wa majengo kwa nguvu za wananchi,tunatarajia  kazi ya kuchimba msingi kukamilisha haraka ili ujenzi uanze rasmi wiki hii”alisema Kaniki.

Ameishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za mradi na mbunge Dkt Homera kwa kusukuma upatikanaji wa fedha za miradi ya mingi ya maendeleo.