Afisa Takwimu kutoka Mfuko wa Utamaduni na Sanaa Tanzania (TACAF) Bw. Shabani Ramadhani Rashidi akitoa mafunzo kuhusu huduma za mfuko huo, kwa wanachama wa Chama cha Wasanii Wachongaji Tanzania (CHAWASAWATA) Mwenge Jijini Dar es Salaam

…………

Mfuko wa Utamaduni na Sanaa Tanzania (TACAF) umeendesha mafunzo ya siku moja kwa Wanachama wa Chama cha Wasanii Wachongaji Tanzania (CHAWASAWATA), kuhusu uelewa wa huduma za mfuko huo.

Mafunzo hayo yalilenga kuwajengea uwezo wasanii wachongaji katika kuboresha kazi zao za sanaa, kuendesha shughuli zao kibiashara, kutambua fursa zilizopo katika sekta ya sanaa, pamoja na kuwawezesha kutumia ipasavyo fursa zinazotolewa na mfuko

Katika mafunzo hayo, chama hicho cha wasanii wachongaji pia kilitoa taarifa ya mwezi mmoja wa utendaji kazi tangu uchaguzi, na mkutano mkuu maalum uliofanyika Julai 12, 2026