
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Mheshimiwa Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo, anatarajiwa kuwasili nchini leo, tarehe 17 Agosti 2026, kwa ziara ya kikazi kufuatia mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Akiwa nchini, Rais Tshisekedi atafanya mazungumzo na mwenyeji wake, Rais Dkt. Samia, ambayo yatajikita katika masuala ya ushirikiano baina ya Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Baada ya mazungumzo hayo, Viongozi hao watazungumza na vyombo vya habari.
Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zina uhusiano wa muda mrefu wa kihistoria na kidugu, unaoendelea kuimarishwa kupitia ushirikiano katika nyanja mbalimbali za maendeleo.
Bakari S. Machumu
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu
