Taasisi ya Elimu Tanzania ( TET) inashiriki kwenye maadhimisho ya wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu 2026 katika viwanja vya Shule ya Sekondari Usagara .
Maadhimisho hayo yameanza leo tarehe 15/08/2026 na kutarajia kumalizika tarehe 24/08/2026, huku kauli mbiu ikiwa “Elimu, Ujuzi na Ubunifu njia ya kufikia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.”
Wadau mbalimbali wameendelea kujitokeza, ambapo Mkurugenzi wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Ladslaus Mnyone akiwa ni miongoni mwao.
Zaidi ya Taasisi 100 kutoka Tanzania Bara na Visiwani zinashiriki maaadhimisho hayo.

