Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akizungumza alipotembelea banda la Kampuni ya Mawasiliano Yas katika Maonesho ya Tamasha la Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, Agosti 12, 2026. Yas ni miongoni mwa wadau muhimu wa Uchumi wa Buluu na maendeleo ya utalii Zanzibar, kupitia uwekezaji wake katika miundombinu ya mawasiliano na huduma za kidijitali zinazochangia kuimarisha muunganisho na ukuaji wa sekta ya utalii visiwani humo.