Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameshiriki katika Tamasha la Usiku wa Kizimkazi “Kizimkazi Festival” lililofanyika tarehe 13 Agosti, 2026 katika kijiji cha Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja.

Aidha, tamasha hilo limehudhuriwa na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Bara, Ndugu Stephen Wasira, pamoja na Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro.