Menejimenti ya Wakala ya Maji na Usafi wa Mazingira (RUWASA) pamoja na Mfuko wa Taifa wa Maji (NWF) Kwa pamoja zimekutana na kujadiliana njia bora za kuwezesha Jumuia za Watumia maji Ngazi ya Jamii ( CBWSO’s ) kuweza kukopa katika mfuko wa Maji ili kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji vijijini ikiwepo kufanya extension ya skimu, ununuzi wa mita na ukarabati miundombinu

Mkutano husika ni kupitia rasimu ya mapendezo ya marekebisho ya kanuni GN Namba 981 ya Mwaka 2019 .

Menejimenti ya taasisi zote mbili zilishiriki katika kikao hicho pamoja na wataalam kutoka Wizara ya Maji na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali .

Aidha , baada ya mapitio hayo ,wajumbe walitoa mapendekezo ili kuwezesha Mfuko wa Taifa wa Maji kuweza kutoa mikopo kwenye vyombo vya watoa huduma za maji ( CBWSO’s).

Mkurugenzi Mkuu wa RUWASA Mhandisi Wolta Kirita pamoja na Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Maji Wakili Haji Nandule Kwa pamoja walikubaliana Kamati ya Mapitio na maboresho kufanyia kazi maeneo yaliyopendekezwa Ili kuwezesha mchakato kuendelea hatua inayofuata