Katika picha ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Aisha Dachi (mwenye fulana yenye milia na mtandio) alipotembelea banda la VETA kwenye Tamasha la Kizimkazi, leo tarehe 13 Agasti, 2026.
Akiwa katika banda hilo amepata taarifa za fursa za mafunzo ya ufundi stadi, lakini pia amepata maelezo kuhusu bidhaa zitokanazo na zao la mwani zinazozalishwa na chuo cha VETA Mtwara kutoka kwa Mkufunzi wa fani ya Upishi Felister Shirima.
Dachi amehitimisha kwa kuipongeza VETA kwa kushiriki katika Tamsha hilo kwani wanachi wanapata taarifa, ufafanuzi na majibu papo kwa hapo.
VETA inashiriki katikaTamasha hilo tangu tarehe 12 Agasti ambapo kilele kinatarajiwa kuwa tarehe 14 Agasti, 2026.

