Mwanasheria Mkuu wa Serikali *Mhe. Hamza S. Johari amewasilisha Maelezo ya Serikali kuhusu Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na.2) wa Mwaka 2026 (The Written Laws (Miscellaneous Amendments ) (No.2) Bill, 2026 kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria tarehe 11 Agosti, 2026 Bungeni Jijini, Dodoma.
Aidha, Mhe. Johari ametoa maelezo ya Serikali kuhusiana na Muswada huo unaolenga kufanya marekebisho katika Sheria kama vile Sheria ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi, Sura ya 166, Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka ya Wilaya) Sura ya 287, Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji), Sura ya 288, Sheria ya Baraza la Usalama la Taifa, Sura ya 61, Sheria ya Uthamini na Usajili wa Wathamini, Sura ya 138 na Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori, Sura ya 283.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria inayoongozwa na Mwenyekiti Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) imepokea na kujadili maelezo Serikali kuhusiana na Muswada huo.

