Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza wananchi Mji Mkongwe (Stone Town) katika eneo la Jaws Corner, Zanzibar, tarehe 10 Agosti, 2026.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na vijana wa Makachu pembezoni mwa bustani ya Forodhani, Zanzibar tarehe 10 Agosti, 2026.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akicheza mchezo wa bao na Bibi Hadia Farhan baada ya kuwasalimia wananchi wa Mji Mkongwe (Stone Town) katika eneo la Jaws Corner, Zanzibar, tarehe 10 Agosti, 2026.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na wananchi wakati akipita kwenye mitaa mbalimbali ya Mji Mkongwe (Stone Town), Zanzibar, tarehe 10 Agosti, 2026.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi ya mfano wa Mlango wa Zanzibar (Zanzibar door) baada ya kuwasalimia wazee wa Mji Mkongwe (Stone Town), Zanzibar, tarehe 10 Agosti, 2026.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi ya mfano wa Jahazi wakati alipowatembelea Wananchi wa Jaws Corner katikati ya Mji Mkongwe, Zanzibar tarehe 10 Agosti, 2026.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisikiliza nyimbo mbalimbali za Taarabu asilia baada ya kuwasili katika eneo la Jaws Corner katikati ya Mji Mkongwe (Stone Town), Zanzibar tarehe 10 Agosti, 2026.