Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametembelea banda la vijana katika kilele cha Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima ya Kimataifa ya Nanenane tarehe 8 Agosti 2026, yanayofanyika katika Viwanja vya Dkt. John Malecela, Nzuguni, jijini Dodoma.
Akiwa katika banda hilo, Mhe. Rais amepata fursa ya kusikilizia na kujionea kazi mbalimbali za ubunifu zinazofanywa na vijana wanaotekeleza Mradi wa BBT kupitia fursa zinazotolewa na Serikali katika Sekta ya Kilimo.
Vijana hao wamemshukuru kwa kuwawezesha kushiriki katika shughuli za kilimo kupitia Mradi wa BBT, wakieleza kuwa fursa hiyo imewasaidia kujiajiri, kuongeza kipato na kuchangia katika maendeleo ya sekta ya kilimo nchini.
Sikukuu ya Wakulima Nanenane 2026 inaongozwa na kaulimbiu: “Tambua Soko; Ongeza Tija Kutekeleza Dira 2050.”
