Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Ngwaru Maghembe amefungua rasmi Maonesho ya 4 ya Bharat Tanzania Mini Defence Expo yaliyoandaliwa na Ubalozi wa India nchini Tanzania tarehe 7 Agosti, 2026. Ufunguzi huo ulihudhuriwa na Balozi wa India nchini Mhe. Bishwadip Dey; Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Luteni Jenerali Salum Othman, Maafisa Jenerali na Maafisa Wakuu wa JWTZ pamoja wawakilishi wa kampuni za utengenezaji wa vifaa vya ulinzi kutoka India.

Katika hotuba yake, Mheshimiwa Naibu Waziri alisisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na India katika Sekta ya Ulinzi, akizihimiza kampuni za India kushirikiana na taasisi za Tanzania ili kukuza biashara, uwekezaji na ubadilishanaji wa teknolojia.

Alieleza kuwa ushirikiano huo utaimarisha uhusiano wa pande mbili, kuongeza uwezo wa Sekta ya Ulinzi na kuchangia kujenga Tanzania yenye usalama zaidi na mazingira bora ya maendeleo.