Kamanda wa Polisi Mkoa wa kipolisi Temeke Kamishna Msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP Kungu John Malulu Julai 28,2026 katika Kata ya Kilungule iliyopo Mbagala Dar es Salaam amemtembelea Ndugu Mustafa aliepoteza watoto watatu kwenye ajali ya Moto iliyotokea Aprili 7,2026

Kabla ya hapo Kamanda Malulu alimshika mkono Mwananchi huyo kwa kumchangia Mifuko ya Saruji na mahitaji mengine muhimu.

Naye Ndug. Hamidu Salum ambaye ni jirani wa familia hiyo amesema Amelishukuru Jeshi la Polisi kupitia kwa RPC Temeke kwa Matendo yake ya huruma kwa familia hiyo, ameomba matendo hayo yawe endelevu kwani yanadumisha mahusiano kati ya Jeshi na Jamii.