Na Baltazar Mashaka, Mwanza
ZAIDI ya wananchi 2,000 mkoani Mwanza wamefaidika na huduma za uchunguzi wa afya ya macho, matibabu na ugawaji wa miwani bila malipo kupitia mradi unaotekelezwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), mkoani humu, ikishirikiana na Christian Social Service Commission (CSSC).

