Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila akipokea maelezo kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Yas, Bw. Pierre Canton Bacara kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo kwenye Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (SABASABA) mara baada ya kutembelea banda hilo.

Banda la Yas limekusanya suluhisho mbalimbali zinazolenga kuboresha maisha ya Watanzania, ikiwemo huduma ya uchunguzi wa macho bure, mpango wa kumiliki simu janja na rauta za 5G kwa mkopo, huduma za intaneti majumbani na kwa wajasiriamali kupitia Yas Fiber, suluhisho kwa wafanyabiashara na taasisi kupitia Yas Business, pamoja na huduma na suluhisho mbalimbali za kifedha kupitia Mixx.