Dar es Salaam, Julai 3, 2026 – Watanzania sasa watapata fursa ya kujishindia simu janja aina ya ZTE A35 kila wiki baada ya Yas Tanzania kuzindua kampeni ya “Register, Login and Win”, inayolenga kuongeza matumizi ya huduma za kidijitali kupitia Yas App.

Kampeni hiyo imezinduliwa leo katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (SabaSaba), ambapo Watanzania wanaotembelea banda la Yas wanaweza kujisajili kwenye Yas App na kuingia moja kwa moja kwenye droo ya kila wiki ya kushinda simu janja aina ya ZTE A35.

Kampeni hiyo itadumu kwa siku 90, huku washindi wanne wakipatikana kila wiki.Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Meneja wa Huduma za Vijana na Wateja Maalum wa Yas Tanzania, Ikunda Ngowi, alisema kampeni hiyo inalenga kuwahamasisha Watanzania kutumia Yas App kupata huduma mbalimbali za mawasiliano kwa urahisi.

“Kupitia Yas App, wateja wanaweza kupata huduma muhimu popote walipo na wakati wowote. Kupitia kampeni hii tunawapa Watanzania sababu zaidi ya kutumia huduma za kidijitali huku tukiwazawadia simu janja,” alisema Ngowi.Aliongeza kuwa kupitia Yas App, wateja wanaweza kununua vifurushi vya intaneti, dakika na SMS, kuangalia salio na kusimamia huduma zao zote za Yas kwa urahisi.

“Tunawaalika Watanzania wote wanaotembelea Maonesho ya SabaSaba kufika banda la Yas, kupakua Yas App na kujisajili ili kupata nafasi ya kushinda simu mpya ya ZTE A35 kila wiki,” alisema.

Naye mmoja wa wateja wa Yas, Julius Mtambalike, aliyekuwa miongoni mwa waliojisajili kwenye Yas App katika banda la kampuni hiyo, alisema kampeni hiyo imempa motisha zaidi wa kutumia huduma za kidijitali.

“Nilikuwa natumia baadhi ya huduma za Yas, lakini kupitia Yas App nimegundua ni rahisi zaidi kujinunulia vifurushi, kuangalia salio na kusimamia huduma zangu zote sehemu moja. Pia kupata nafasi ya kushinda simu janja ni motisha nzuri kwa wateja kama sisi kutumia teknolojia zaidi,” alisema Mtambalike.

Kupitia kampeni hiyo, Yas inalenga kuongeza matumizi ya huduma za kidijitali, kurahisisha upatikanaji wa huduma za mawasiliano na kuwahamasisha Watanzania kutumia teknolojia katika maisha yao ya kila siku.