Timu ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Watumishi Housing Investments (WHI) ipo katika ziara ya kukagua miradi ya ujenzi wa nyumba za Watumishi ambapo leo tarehe 28 Juni, 2026 imekagua maendeleo ya mradi wa Ujenzi wa nyumba ya Watumishi 6:1 katika Shule ya Sekondari Samia Suluhu Hassan – Ruangwa, pamoja na mradi wa Ujenzi wa Nyumba ya Watumishi 3:1 katika Kituo cha Afya Mtandi , Masasi-Mtwara.