
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akimsikiliza Afisa wa Tiba Bi. Rehema Ramadhan akielezea utendaji kazi wa mashine ya kutibu saratani (Linear Accelerator) baada ya kuzindua Jengo la Kitengo cha Tiba ya Mionzi katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini (KCMC), Moshi mkoani Kilimanjaro, tarehe 24 Juni, 2026.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akipokea Tuzo ya Heshima kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini (KCMC), ambaye pia ni Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dkt. Alex Gehaz Malasusa, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Jengo la Tiba ya Upasuaji katika viwanja vya hospitali hiyo, Moshi mkoani Kilimanjaro, tarehe 24 Juni, 2026.

