Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiagana na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Namibia Mhe. Dkt, Netumbo Nandi-Ndaitwah katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 22 Juni, 2026. Rais Mhe. Dkt. Ndaitwah amehitimisha Ziara yake ya Kitaifa ya siku 4 nchini Tanzania ambapo pamoja na kufanya mazungumzo na Rais Mhe. Dkt. Samia pia alitembelea Kambi ya Kihistoria ya Wapigania Uhuru wa nchi yake, Kongwa mkoani Dodoma.

RAIS DKT. SAMIA AMUAGA RAIS WA NAMIBIA DKT. NETUMBO NDAITWAH
