Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) Mhe. Prof. Riziki Shemdoe akitoa maelekezo kwa Mkandarasi kampuni ya China Railways and Bridges Corporation (CRBC), wakati wa ziara yake ya kukagua barabara zinazojengwa kupitia Mradi wa Uboreshaji wa Jiji la Dar es Salaam Awamu ya Pili (DMDP II) katika Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) Mhe. Prof. Riziki Shemdoe akisisitiza jambo kwa Mkandarasi kampuni ya China Railways and Bridges Corporation (CRBC), wakati wa ziara yake ya kukagua barabara zinazojengwa kupitia Mradi wa Uboreshaji wa Jiji la Dar es Salaam Awamu ya Pili (DMDP II) katika Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya wa Ubungo Mhe. Albert Msando akitoa ufafanuzi wa jambo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) Mhe. Prof. Riziki Shemdoe, wakati wa ziara ya kikazi ya waziri huyo ya kukagua barabara zinazojengwa kupitia Mradi wa Uboreshaji wa Jiji la Dar es Salaam Awamu ya Pili (DMDP II) katika Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Miradi ya Ushirikiano na Benki ya Dunia Mhandisi Humprey Kanyenye wa TARURA akifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) Mhe. Prof. Riziki Shemdoe, wakati wa ziara ya kikazi ya waziri huyo ya kukagua barabara zinazojengwa kupitia Mradi wa Uboreshaji wa Jiji la Dar es Salaam Awamu ya Pili (DMDP II) katika Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Ubungo akisikiliza maelezo ya Mkandarasi kampuni ya China Railways and Bridges Corporation (CRBC), wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI Mhe. Prof. Riziki Shemdoe ya kukagua barabara zinazojengwa kupitia Mradi wa Uboreshaji wa Jiji la Dar es Salaam Awamu ya Pili (DMDP II) iliyofanyika katika Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Mkandarasi kampuni ya China Railways and Bridges Corporation (CRBC) akitoa ufafanuzi wa sababu ya kususua kwa ujenzi wa barabara kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu –TAMISEMI Mhe. Prof. Riziki Shemdoe wakati wa ziara ya waziri huyo ya kukagua barabara zinazojengwa kupitia Mradi wa Uboreshaji wa Jiji la Dar es Salaam Awamu ya Pili (DMDP II) katika Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Mshauri Elekezi kutoka kampuni ya NIMETA Consult (T) akieleza changamoto za mkandarasi kampuni ya China Railways and Bridges Corporation (CRBC) kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu -TAMISEMI Mhe. Prof. Riziki Shemdoe wakati wa ziara ya waziri huyo ya kukagua barabara zinazojengwa kupitia Mradi wa Uboreshaji wa Jiji la Dar es Salaam Awamu ya Pili (DMDP II) katika Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es Salaam.
Mkazi wa Sinza Bw. Jawa Waziri akimshukuru Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI Prof. Riziki Shemdoe kwa kufanya ziara ya ukaguzi wa barabara ya mtaa anaoishi wa Sinza Lion na kumpongeza kwa kumuelekeza mkandarasi CRBC kukamilisha kwa wakati barabara hiyo ambayo imekuwa ni kero kwa wakazi wa eneo hilo.
Mwonekano wa moja wa mtaro wenye changamoto ya kujaa maji katika barabara ya Mtaa wa Lion uliopo Sinza wilayani Ubungo, ambao unakarabatiwa kupitia utekelezaji wa Mradi wa Uboreshaji wa Jiji la Dar es Salaam Awamu ya Pili (DMDP II).
…………..
Na OWM – TAMISEMI, Dar es Salaam
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) Mhe. Prof. Riziki Shemdoe ametaka Mkandarasi kampuni ya China Railways and Bridges Corporation (CRBC) inayojenga barabara tisa (9) za lami zenye urefu wa kilometa 5.42 kukamilisha ujenzi wa barabara saba (7) zilizosalia ifikapo Agosti 14, 2026, barabara hizo zinajengwa kupitia Mradi wa Uboreshaji wa Jiji la Dar es Salaam Awamu ya Pili (DMDP II) katika kata za Sinza, Mburahati, Mabibo na Makurumla wilayani Ubungo.
Prof. Shemdoe ametoa maelekezo hayo Juni 13, 2026 Katika Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua ujenzi wa barabara 23 zenye urefu wa kilometa 52.37 zinazojengwa wilayani Ubungo katika kata 11 kupitia utekelezaji wa Mradi wa Uboreshaji wa Jiji la Dar es Salaam Awamu ya Pili (DMDP II).
Prof. Shemdoe amesitiza kuwa, mkandarasi huyo anayesuasua katika ujenzi wa barabara hizo kwa kisingizio cha lami kuchelewa kufika kutokana na vita ya Mashariki ya Kati, hatopewa muda wa nyongeza wa kukamilisha ujenzi wa barabara hizo iwapo atashindwa kukamilisha ifikapo Agosti 14, 2026 kwa mujibu wa mkataba.
“TARURA hakuna kumuongezea muda mkandarasi huyu, atafute lami popote atakapoipata na afanye kazi usiku na mchana kukamilisha barabara hizi 7 zilizosalia ili kuwaondolea adha wananchi,” amesisitiza Prof. Shemdoe.
Katika kuhakikisha barabara zinakamilika kwa wakati, Prof. Shemdoe ameitaka TARURA na Mshauri Elekekezi (NIMETA Consult (T) kumshauri mkandarasi CRBC kwa kuangalia uwezekano wa kukabidhi baadhi ya barabara hizo kwa mkandarasi mwingine (sub contract) ili ujenzi ukamilike kwa wakati.
Aidha, Prof. Shemdoe amemuelekeza Mtendaji Mkuu wa TARURA Mhandisi Victor Seff kumuondoa Mkuu wa Kitengo cha Fedha na Uhasibu Bw. Evans Mgeusa anayesimamia Fedha za Miradi ya Benki ya Dunia kwa kitendo cha kuchelewesha malipo na kumleta mwingine ambaye atafanya kazi kwa weledi na wakati.
Sanjari na hilo, Prof. Shemdoe amemuelekeza Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI Bw. Adolf Ndunguru kuwaondoa Wahasibu Bw. Julius Bashuta na Mbwana Mkembe wa kitengo hicho cha Fedha na Uhasibu kinachosimamia fedha za miradi ya Benki ya Dunia, na kuwaleta wengine ambao watafanya kazi vizuri na kwa uaminifu.
Akizungumzia jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita, Prof. Shemdoe amempongeza Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha utiaji saini wa mikataba minne ya ujenzi wa barabara za wilaya ya Ubungo yenye thamani ya shilingi bilioni 77, 457,169,172.73 kupitia Mradi wa Uboreshaji wa Jiji la Dar es Salaam Awamu ya Pili (DMDP II).
Kwa upande wake Mkazi wa Sinza Bw. Jawa Waziri amemshukuru Prof. Shemdoe kwa kufanya ziara ya ukaguzi wa barabara ya mtaa wake wa Sinza Lion na kumpongeza kwa kumuelekeza mkandarasi CRBC kukamilisha kwa wakati barabara hiyo ambayo imekuwa ni kero kwa wakazi wa eneo hilo.
