Kamishna wa Uhifadhi, Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro Abdul-Razaq Badru ameongoza mbio za Fame Marathon zilizofanyika leo tarehe 14 Juni, 2026 katika mji wa Karatu mkoani Arusha.
Mbio hizo zilizokuwa na umbali wa Kilomita 21, 10, 05 na 02 zimeratibiwa na Hospitali ya Fame iliyopo Karatu na kuhusisha takribani wakimbiaji 650 kutoka ndani na nje ya Nchi.
Akizungumza wakati wa Uzinduzi wa mbio hizo Kamishna Badru ameeleza kuwa Uhifadhi endelevu ni pamoja na kushirikiana na Jamii zinazozunguka hifadhi katika programu ambazo zina manufaa kwa Jamii na kutoa tabasamu kwa wagonjwa mbalimbali wanaopata huduma kwenye Hospitali na Fame na nyinginezoÂ
Mkurugenzi wa Uendeshaji kutoka Hospitali ya FAME Bw. William Mhapa ameleeleza kuwa mbio hizo zinafanyika kwa mara ya tatu kwa lengo kushirikiana na jamii kuchangia mahitaji mbalimbali ya wagonjwa wanaofikishwa hospitali ya FAME kupata huduma za dharura na kutoa msaada kwa jamii za Karatu, Ngorongoro na maeneo jirani

