Na Victor Masangu, Kibaha
Madiwani wa chama cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani wametakiwa kujenga mising imara iya kuwa na uzalendo na Taifa lao ikiwa  pamoja na kuweka mikakati  kabambe ya kupambana na kero na chanagamoto mbali mbali za wananchi ili kuweza kuzitafuta ufumbuzi.

Hayo yamebainishwa na  Mjumbe wa halmashauri kuu ya (CCM) Taifa  Mohamed Mchengerwa (MNEC)  ambaye pia ni  Waziri wa afya wakati   wa kufungua mafunzo maalumu kwa madiwani wa CCM Mkoa wa Pwani  ambayo yamefanyika katika shule ya uongozi ya Mwalimu Julias Nyerere iliyopo eneo la kwa mfipa katika  Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha Mkoa wa Pwani.

Mchengerwa amesema kwamba  mafunzo hayo  kwa madiwani wa Mkoa wa Pwani  watawajengea uwezo mkubwa katika suala zima  la kuwatumikia wananchi wao ikiwemo kusikiliza kero na  changamotto mbali mbali ambazo  zinawakabili  wanapaswa kuwa wazalendo.
Kadhalika Mchengerwa amesema kwamba madiwani wanapaswa kuabdilika na kuwa mstari wa mbele katika kwenda  kuwa suluhisho  katika  kuwasikiliza wananchi na kushirikiana nao katika mambo mbali ya kijamii.
“Kwanza kabisa nipende kuchukua fursa hii kumpongeza kwa dhati kabisa Katibu wa chama caha mapinduzi (CCM)  kwa kuweza kuwakutanisha kwa mara ya kwanza madiwani wote wa CCM  wa Mkoa wa Pwani kwa hivyo kitu kikubwa ninachowaomba ni kuwa wazalendo na nchi yao na kuelekeza nguvu zao katika kutatua kero na changamoto za wananchi,”amebainisha Mchengerwa.
Pia Mchengerwa hakusita kugusia suala la madiwani hao kuwa na upendo, na mshikamano wa pamoja katika maeneo yao kwa lengo la kuweza kushirikiana bega kwa bega na wananchi kwa ajili ya kuweza kuwaletea maendeleo chanya.

Kwa uppande wake Katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani Ndg. Kiite Mfilinge amesema kwamba lengo kubwa la mafunzo hayo ni kuwakutanisha madiwani hao ili kuwajengea uwezo  ikiwa  pamoja  na kuwakumbushia kutekeleza  majukumu yao pamoja na kuwahudumia wananchi.

Katibu huyo amefafanya kwamba katika mafunzo hayo jumla ya madiwani wote  wapatao 185 wameweza kupata fursa ya kushiriki na  kwamba wamejifunzo mada mbali mbali ikiwemo suala la uzalendo, uwajibikaji, ulinzi na usalama ikiwa pamoja na kuwa na dira ya pamoja katika ngazi ya Mkoa ambayo itaweza kuleta matokeo ya namna bora ya kuwatumikia wannchi.

Kwa upande wake Mwalimu wa shule ya uongozi mwalimu Julias nyerere Profesa Mercellina Chijoriga ambaye pia alikuwa mtoa  mada katika mafunzo hayo amesema amebainisha kuwa mafunzo hayo yataweza kuleta tija zaidi ya uwajibikaji katika suala zima la kuwahudumia wananchi katika maeneo yao.

Pia Profesa huyo ametumia mafunzo hayo kuwahimiza   madiwani  wa Mkoa wa Pwani kuzingatia  kwa weledi na ufanisi mkubwa dira ya Taifa  ambayo itaweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa kutimiza majukumu yao ipasavyo ikiwemo suala zima la utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Nao baadhi ya madiwani ambao wamehudhuria katika mafunzo hayo akiwemo Ally Simba Diwani wa Kata ya Misusugu pamoja na Diwani wa Kata ya Mwewe omary Msombwe wameahidi kwenda kuyatumia vema mafunzo hayo ambayo wameyapata na kwamba  yameweza kuwajengea uwezo mkubwa katika kutekeleza majukumu yao.

Mafunzo hayo ya siku moja yamewajumuisha madiwani wote wa Mkoa wa Pwani waoatao 185 ambapo wamepata fursa ya kujifunz amada mbali  mbali ikiwemo suala la uzalendo, ulinzi na amani, uwajibikaji kwa wananchi wao , jinsi ya kusimamia mapato, na kujifunza mambo mbali mbali amabyo yataweza kuwa ni mkombozi mkubwa katika maeneo yao.