Na. Ssgt Mawazo Mtondo – Dodoma.
Kamishna wa Huduma za Urekebu Jeshi la Magereza, CP Amina Kavirondo, alisema Jeshi la Magereza limejipanga kutumia mifumo mbalimbali ya kidijitali ili kuachana na mifumo ya zamani na kwenda sambamba na maendeleo ya teknolojia katika utekelezaji wa majukumu yake.
CP. Kavirondo alisisitiza kuwa maafisa na askari wa Jeshi la Magereza wana wajibu wa kuendeleza na kuboresha mifumo iliyopo kwa kutumia rasilimali zilizopo, ili kufanikisha dhana ya urekebishaji kwa ufanisi zaidi.
Alitoa kauli hiyo Juni 10, 2026, wakati akiwasilisha mada mbalimbali ikiwemo Dhana ya Urekebishaji na Mtazamo wa Haki za Binadamu katika Mafunzo kwa Maafisa Ustawi wa Jamii kuhusu Mwongozo wa Utekelezaji wa Programu za Urekebishaji. Mafunzo hayo yanaendelea kufanyika katika Ukumbi wa Rugimbana, Msalato, jijini Dodoma, na yanatarajiwa kuhitimishwa Juni 12, 2026.

