Na Prisca Libaga RS Arusha
Mashindano ya Michezo kwa Shule za Sekondari (UMISSETA) Mkoa wa Arusha yameanza rasmi katika viwanja vya Shule ya Sekondari Ilboru, yakishirikisha zaidi ya wanamichezo 700 kutoka halmashauri zote saba za mkoa huo.
Akizungumza wakati wa kuanza kwa mashindano hayo, Mratibu wa UMISSETA Mkoa wa Arusha, Daniel Nanyaro, amesema mashindano hayo yanahusisha michezo mbalimbali yenye lengo la kuibua, kukuza na kuendeleza vipaji vya wanafunzi.
Aidha, wadau wa michezo pamoja na wanafunzi walioshiriki wameeleza matumaini yao kuwa mashindano hayo yatasaidia kuinua kiwango cha michezo shuleni na kutoa fursa kwa vipaji vya vijana kuonekana na kuendelezwa.

