‎Na Prisca Libaga RS ARUSHA

Watumishi wa kada ya chini katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha wameishukuru Serikali ya Mkoa huo kwa kuwawezesha kushiriki mafunzo ya kuwajengea uwezo na kuongeza ufanisi katika utendaji wa kazi.

‎Watumishi hao wamempongeza Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Dkt. Toba Nguvula, kwa kutambua mchango wao na kugharamia ushiriki wao katika mafunzo hayo yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam.

‎Aidha, wameeleza kuwa kwa mara ya kwanza wamepata fursa ya kusafiri kwa ndege ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kutoka Arusha kupitia Zanzibar hadi Dar es Salaam, hatua waliyoitaja kuwa motisha kubwa katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

‎Wamesema mafunzo hayo yamewaongezea maarifa, ujuzi na ari ya kazi, hivyo kuwasaidia kuboresha huduma wanazotoa kwa wananchi.