Na John Walter -Kondoa
Mwenge wa Uhuru mwaka 2026 umewasili katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma ambapo jumla ya miradi 14 yenye thamani ya shilingi bilioni 3.9 inatarajiwa kukaguliwa, kuwekwa mawe ya msingi pamoja na kuzinduliwa.
Miradi hiyo inalenga kuboresha huduma za kijamii na kuongeza ustawi wa wananchi wa Wilaya ya Kondoa.
Mwenge huo umepokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Fatma Almas Nyangasa ukotokea Wilaya ya Bahi.
Kwa upande wake, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2026, Wazo Michael Mwang’onda amewataka wazazi nchini kuwalea watoto wao katika maadili mema ili kujenga jamii yenye heshima na uwajibikaji.
Aidha, amewahimiza vijana kuwa wazalendo kwa nchi yao kwa kushiriki shughuli za maendeleo na kulinda tunu za Taifa.
Kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru mwaka 2026 inasema; “Tanzania ni yetu sote, tushikamane kwa pamoja kuleta maendeleo.”