Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi, leo tarehe 29 Mei, 2026 amewasilisha Randama ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027 mbele ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya utekelezaji wa mipango na vipaumbele vya wizara kwa mwaka ujao wa fedha.