Na. Meleka Kulwa-Fullshangwe Blog, Bungeni Dodoma
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Mei 29, 2026 limepitisha jumla ya Shilingi bilioni 210.2 kwa ajili ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kutekeleza majukumu yake katika mwaka wa fedha 2026/2027.
Fedha hizo zinajumuisha Shilingi bilioni 100.2 kwa matumizi ya kawaida na Shilingi bilioni 110 kwa utekelezaji wa miradi ya maendeleo
Akiwasilisha jana Mei 28,2026 makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo bungeni jijini Dodoma, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Leonard Akwilapo, alisema fedha hizo zitaelekezwa katika kuimarisha huduma za ardhi, upimaji wa viwanja, upangaji miji, utatuzi wa migogoro ya ardhi pamoja na kuendeleza mifumo ya kidijitali ya e-Ardhi.
Aidha, kati ya fedha za maendeleo, Shilingi bilioni 44.1 zitatokana na vyanzo vya ndani na Shilingi bilioni 65.9 kutoka vyanzo vya nje kwa ajili ya kusaidia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ya sekta ya ardhi nchini.
