Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Benjamin Kuzaga leo Mei 26, 2026 amempongeza kwa kumpaKAMANDA KUZAGA AMPONGEZA ASKARI ALIYEOKOA MAISHA YA DEREVA BODABODA cheti cha pongezi Konstebo wa Polisi Baraka Wambura Nyakarungu kwa kitengo cha ujasiri alichofanya na kuokoa maisha ya mhanga wa ajali ya Pikipiki.
Konstebo wa Polisi Nyakarungu mnamo Mei 14, 2026 majira ya saa 12 alfajiri akiwa kwenye Daladala akitokea kazini kuelekea nyumbani alipofika eneo la Kilimo Uyole alikuta ajali iliyohusisha Gari ya abiria na Pikipiki na kumchukua majeruhi, kumfikisha kituo cha Polisi Uyole kwa ajili ya kupatiwa PF3 na kisha kumfikisha katika Hospitali ya Igawilo kwa matibabu.
Mhanga wa ajali hiyo alipatiwa matibabu na kwa sasa anaendelea vizuri. Jeshi la Polisi lina thamini na kutambua kazi mbalimbali zinazofanywa na Askari kwa kuzingatia Nidhamu, Haki, Weledi na Uadilifu.

