WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza ambapo anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika kilele cha maadhimisho ya kwanza ya Siku ya Ziwa Victoria yatakayofanyika katika viwanja vya Nanenane Nyamhongolo jijini Mwanza.
Maadhimisho hayo yanaongozwa na kauli mbiu isemayo: “Maji Yetu, Mustakabali Wetu: Tuungane kwa Uendelevu wa Bonde la Ziwa Victoria.”
Katika uwanja wa ndege wa Mkoa wa Mwanza, Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu amepokelewa na viongozi mbalimbali, wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda na Waziri wa Maji Jumaa Aweso.

