Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, leo tarehe 15 Mei 2026 amewasili mkoani Mara kwa shughuli za Kikazi. Pamoja na mambo mengine Mhe. Makamu wa Rais anatarajiwa kushiriki Mazishi ya Bw. Boniface Makene, aliyewahi kuwa Mwandishi wa Habari wa Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mohamed Gharib Bilal, yatakayofanyika katika Kijiji cha Mabui, Musoma Vijijini mkoani Mara, kesho tarehe 16 Mei 2026.