Na Victor Masangu, Kibaha
Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha katika kumuunga mkono Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuleta chachu ya maendeleo imeamua kutumia fursa ya makusanyo ya fedha za mapato yake ya ndani katika kuhakikisha inakabiliana na changamoto mbali mbali zinazowakabili wananchi ikiwemo suala la kuboresha  miundombinu ya  barabara za mitaa zilizopo katika kata zote 14.
Hayo yamebainishwa na Mstahiki meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha Dr. Nicas Mawazo wakati wa kikao cha kikanuni cha  baraza la madiwani robo ya tatu  ya kuanzia mwezi januari mwaka huu wa 2026 hadi kufikia Machi ambapo amebaini lengo kubwa ni kuhakikisha wanawaletea mabadiliko chanya ya kimaenndeleo katika nyanja mbali mbali kupitia mapato ya ndani.
Mstahiki Meya amebainisha kwamba katika kikao hicho wamemeweza kupata fursa ya kupokea taarifa mbali mbali kutoka katika baadhi ya taasisi ikiwemo Dawasa, Tanesco, Bima ya afya, Tarura, pamoja na nyinginezo kwa lengo la kujadili mambo mbali mbali ambayo yataweza kuletaa tija zaidi katika kutatua changamoto mbali mbali za wananchi katika maeneo ambayo wanaishi.
“Tumefanya  kikao chetu cha kikanuni cha baraza letu la  madiwani   na kwamba tumejadili mambo mbali mbali ikiwemo suala la  upatikanaj  wa huduma ya maji safi na salama, kuboresha miooundombinu ya barabara za mitaa ambapo tumeweza kutenga kiasi cha shilingi milioni 50 kwa kila mtaa na hii itaweza kusaidia kwa kiais kikubwa katika kuboresha miundombinu ya barabara sekta ya elimu na afya ,”amebainisha  Dr. Nicas.
Kwa upande  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha Dkt. Rogers Shemwelekwa amesema kwamba lengo kubwa niu kuzidi kuendelea kuongeza kasi zaidi katika suala zima  ukusanyaji wa mapato ya ndani ambayo pia yataweza  kusaidia  katika  kutekeleza  baadhi ya miradi mbali mbali ya maendeleo.
Shemwelekwa  ameahidi kuendelea kushirikiana bega kwa bega na viongozi pamoja na  madiwani kwa lengo la kuweza   kuleta dhana pana ya ushirikishwaji  ambayo   itaweza  kuleta matokeo chanya kataika suala zima la maendeleo.
Nao baadhi ya madiwani wa viti maalumu akiwemo Selina Wilson katika kupambana naa maambukizi mapya ya virusi vya ukimvi (VVU) hakusita kuwahimiza wakinababa kutumia kinga kwa lengo la kuweza kuepukana na maambukizi mapya na kwamba ni vema sasa kuwahimiza umuhimu wa kutumia kondomu katika tendo la ndoa na kuacha na ngono zembe.
Naye Diwani wa viti maalumu Shufaa Mshana pamoja na Sara  Uledi wamesema wameomba juhudi za makusudi zifanyika katika kuboresha sekta ya afya hasa kwa upande wa wakinamama wajawazito ambao wamekuwa wakitembea umbari mrefu katika baadhi ya maeneo kwa ajili ya kwenda  kupata huduma ya kujifungua.
Kikao cha kikanuni  cha baraza la madiwani robo ya tatu ya kuanzia Januari hadi machi mwaka huu kimeweza kujadili mambo mbali mbali ikiwemo suala la kuimarisha miundombinu ya barabara za mitaa, kuboresha huduma ya maji safi na salama, upatikanaji wa bima ya afya kwa wote, suala la afya, elimu  pamoja na mambo  mengine yaa msingi kwa ajili ya maslahi ya wananchi kwa ujumla.