Matukio mbalimbali katika picha ni wakufunzi 25 wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) wakiongozana na watumishi kutoka Kitengo cha Mafunzo Makao Makuu, leo Mei 10, 2026 wakiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salaam, tayari kwa safari ya kwenda nchini Finland kujifunza teknolojia na ujuzi unaohitajika katika uchimbaji pamoja na ukuzaji wa mnyororo wa thamani wa madini.

Mafunzo hayo yanafanyika kupitia mradi wa Vocational Pathway to Sustainable Critical Raw Minerals in Tanzania, unaolenga kuimarisha elimu ya ufundi stadi katika sekta ya madini nchini, kwa ufadhili wa Umoja wa Ulaya (EU).