Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb) amewasili jijini Djibouti, Jamhuri ya Djibouti kwaajili ya kumuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye sherehe za Uapisho wa Rais Mteule wa nchi hiyo Mhe. Ismaïl Omar Guelleh.

Mheshimiwa Kombo amewasili jijini hapa Tarehe 08 Mei, 2026 kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Djibouti-Ambouli na kupokelewa na Waziri wa Bajeti wa nchi hiyo Mhe. Isman Ibrahim Robleh.

Mheshimiwa Waziri Kombo anatarajiwa kushiriki katika sherehe hizo za uapisho wa Rais Mteule wa Jamhuri ya Djibouti Mhe. Ismail Omar Guelleh zinazotarajiwa kufanyika jijini hapa leo Mei 09, 2026 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Djibouti akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Rais Mteule wa Djibouti Mhe. Ismaïl Omar Guelleh amechapguliwa kuongoza nchi hiyo kwa muhula wa sita mfululizo kufuatia ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika Tarehe 10 Aprili, 2026 nchini humo.