Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea Tuzo ya kuwa Kinara wa Dhana ya Urekebishaji wa Wafungwa Magerezani kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Patrobas Paschal Katambi kwenye hafla ya hafla ya kuhitimisha Mafunzo ya Uongozi Ngazi ya Juu Kozi namba 28 na Uongozi Daraja la Pili Kozi namba 48 ya mwaka 2025/2026 katika Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania (TCT) Ukonga Jijini Dar es Salaam tarehe 09 Mei, 2026.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mfungwa Bw. Lista Chisoma ambaye amepata ujuzi wa kushona bidhaa mbalimbali za ngozi na vitambaa wakati akiwa gerezani, katika Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania (TCT) Ukonga Jijini Dar es Salaam tarehe 09 Mei, 2026.
Kikundi cha burudani cha wafungwa na Askari Magereza kikitumbuiza katika hafla ya kuhitimisha Mafunzo ya Uongozi Ngazi ya Juu Kozi namba 28 na Uongozi Daraja la Pili Kozi namba 48 ya mwaka 2025/2026 katika Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania (TCT) Ukonga Jijini Dar es Salaam tarehe 09 Mei, 2026.
…………..
Na. John Bukuku- Dar es salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali itaendelea kuimarisha mfumo wa urekebishaji wa wafungwa nchini ili kuwajengea uwezo wa kujitegemea baada ya kumaliza vifungo vyao.
Aidha, Amesema kuwa Jeshi la Magereza lina jukumu kubwa katika mfumo wa haki jinai nchini kupitia usimamizi wa mahabusu na wafungwa pamoja na utekelezaji wa programu za urekebishaji wa tabia.
Ameyasema hayo Mei 9, 2026 wakati akihitimisha Mafunzo ya Uongozi Ngazi ya Juu Kozi Na. 28 na Uongozi Daraja la Pili Kozi Na. 48 kwa mwaka 2025/2026 yaliyofanyika Ukonga jijini Dar es Salaam.
Aidha amesema Serikali imeendelea kufanya mageuzi katika mfumo wa magereza kwa kuweka mkazo kwenye mafunzo ya ufundi stadi, kilimo, ufugaji na shughuli nyingine za uzalishaji kwa wafungwa ili kuwajengea uwezo wa kujitegemea wanaporejea kwenye jamii. akisema kuwa
” nimetembelea mabanda ya maonesho na kushuhudia kazi mbalimbali zinazofanywa na wafungwa ikiwemo ushonaji wa nguo, utengenezaji wa viatu, useremala, ufugaji wa nyuki pamoja na uzalishaji wa maziwa na bidhaa zake” amesema Rais Samia
Aidha, amesema changamoto kubwa inayowakabili wafungwa wanaomaliza vifungo ni ukosefu wa mtaji wa kuanzia maisha mapya licha ya kuwa na ujuzi wa kazi mbalimbali walioupata magerezani, huku akibainisha kuwa Serikali inaanza kufikiria uwepo wa mfuko maalumu wa kuwawezesha wafungwa wanaomaliza vifungo ili waweze kuanza shughuli za uzalishaji na kujiepusha kurejea kwenye vitendo vya uhalifu.
Amesema kuwa baadhi ya wafungwa wanaorejea magerezani hufanya hivyo kutokana na kukosa sehemu ya kuanzia maisha baada ya kutoka gerezani.
Rais Samia ameongeza kuwa ni muhimu kuwepo kwa mfumo wa kidigitali wa ufuatiliaji na tathmini kwa wafungwa wanaomaliza vifungo ili kufahamu maendeleo yao pamoja na namna wanavyotumia ujuzi walioupata.
Aidha amesema hatua zinazochukuliwa na Jeshi la Magereza zinaendana na utekelezaji wa Ajenda ya Taifa ya Maendeleo 2050 pamoja na malengo ya kimataifa ya kuimarisha amani, haki na taasisi imara.
Pia, Rais Samia amewapongeza wahitimu wa mafunzo hayo kwa nidhamu, ustahimilivu na utulivu walioonesha katika kipindi chote cha mafunzo., Ambapo mafunzo hayo yamehusisha wanafunzi 659 huku wahitimu 15 wakitoka Chuo cha Mafunzo Zanzibar jambo alilosema linaimarisha ushirikiano na kubadilishana uzoefu kati ya Tanzania Bara na Zanzibar visiwan
Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi amesema Serikali imeendelea kuboresha mazingira ya kazi kwa vyombo vya ulinzi na usalama kupitia ujenzi wa miundombinu, ununuzi wa magari pamoja na kuongeza ajira kwa askari wapya.
Aidha amesema Serikali imeendelea kutekeleza mapendekezo ya Tume ya Haki Jinai ikiwemo kupunguza msongamano magerezani kupitia utoaji wa misamaha kwa wafungwa pamoja na matumizi ya adhabu mbadala nje ya magereza.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP) Jeremiah Yoram Katungu amesema maboresho yaliyofanywa na serikali ya Samia Suluhu Hassan ndani ya Jeshi la Magereza yameendelea kuleta mabadiliko makubwa katika utoaji wa haki na ustawi wa wafungwa nchini.
Akizungumza mbele ya Rais Samia katika hafla ya kufunga Mafunzo ya Uongozi Ngazi ya Juu Kozi namba 28 iliyofanyika Ukonga Magereza jijini Dar es Salaam Mei 09, 2026, Katungu alisema serikali imeendelea kuboresha mazingira ya magereza pamoja na kuongeza fursa za marekebisho kwa wafungwa kupitia elimu na mafunzo mbalimbali ya stadi za kazi.
Alisema hatua ya baadhi ya wafungwa waliokuwa wamehukumiwa adhabu ya kunyongwa kubadilishiwa hukumu zao na kuwa kifungo cha maisha imeongeza matumaini kwa wafungwa wengi huku wengine wakipata nafasi ya kutumikia vifungo vya nje kutokana na mwenendo wao mzuri na mabadiliko ya kitabia.
Katungu alieleza kuwa kuundwa kwa Tume ya Haki Jinai kumeendelea kusaidia maboresho katika mfumo wa utoaji haki nchini kwa kupunguza changamoto za ucheleweshaji wa kesi pamoja na msongamano wa wafungwa na mahabusu magerezani.
Aidha, alimpongeza Rais Samia kwa kuendelea kuliwezesha Jeshi la Magereza kupitia maboresho ya miundombinu, huduma za afya pamoja na mafunzo kwa askari wa magereza, hatua ambayo amesema imeongeza ufanisi wa utendaji kazi na kuimarisha huduma za marekebisho nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiangalia kiatu ambacho kimetengenezwa na Kiwanda cha viatu cha Gereza la Karanga, Moshi mkoani Kilimanjaro wakati alipotembelea mabanda ya maonesho katika Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania (TCT) Ukonga Jijini Dar es Salaam tarehe 09 Mei, 2026.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mfungwa Bw. Lista Chisoma ambaye amepata ujuzi wa kushona bidhaa mbalimbali za ngozi na vitambaa wakati akiwa gerezani, katika Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania (TCT) Ukonga Jijini Dar es Salaam tarehe 09 Mei, 2026.



Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye hafla ya kuhitimisha Mafunzo ya Uongozi Ngazi ya Juu Kozi namba 28 na Uongozi Daraja la Pili Kozi namba 48 kwa Mwaka 2025/2026 katika Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania (TCT) Ukonga Jijini Dar es Salaam tarehe 09 Mei, 2026.
Kikundi cha Wanawake wa Jeshi la Magereza kikionesha onesho Maalumu katika uwanja wa Gwaride wakati wa kuhitimisha Mafunzo ya Uongozi Ngazi ya Juu Kozi namba 28 na Uongozi Daraja la Pili Kozi namba 48 kwa Mwaka 2025/2026, tarehe 09 Mei, 2026.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mfungwa Bi. Grace Chiduo na Bi. Irene Mseluka ambao wamepata ujuzi wa kushona bidhaa mbalimbali akiwa gerezani katika Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania (TCT) Ukonga Jijini Dar es Salaam tarehe 09 Mei, 2026.
