Na WMJJWM – Dar es Salaam
Waandaaji wa vipindi vya watoto wamehimizwakutumia taaluma zao na lugha rafiki kwa watoto na vijana pamoja nakuzingatia maadili ya taaluma ya Habari katika kuandaa maudhui yenyeubora yatakayochangia ukuaji na maendeleo ya mtoto katika jamii.
Hayo yamesemwa na Mratibu wa Programu ya malezi na familia kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Victor RugalabamuMei 8, 2026 wakati wa kuhitimisha mafunzo maalum yaliyoandaliwa na Wizara hiyo kwakushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumiawatoto (UNICEF) kwa lengo la kuwajengea uwezo waandaaji wa vipindi wa radio zajamii, Televisheni na Mitandao ya Kijamii katika kutengeneza maudhuiyanayofundisha, kuburudisha na kuhamasisha maadili mema kwa watoto.
Victor amesema, kupitia mafunzo hayo, Wizara inatarajia kuona vipindi vitakavyorushwa kupitia vyombo vya habari vinatoa mafunzo yamaadili mema kwa kizazi cha sasa na kijacho pia vinahamasishamalezi mazuri ndani ya familia na kuwasaidia watoto na vijanabalehe kukua katika mazingira salama, yenye upendo na ulinzi.
Kwa upande wake Mwezeshaji wa mafunzo hayo,Sabrina Majikata kutoka Shirikia Lisilo la Kiserikali la ICS amesemamafunzo yamejikita kuwawezesha Waandishi wa Habari katika kutayarishavipindi bora na kuzungumza kwa ufasaha katika nguzo tatu ambazo ninamna ya mzazi kumjali, kumtunza nakuzungumza na mtoto ili aweze kubaini changamoto zinazoweza kuathiri maendeleo yake.
“Mwandishi wa habari anapokuwa na uelewa kuhusu ukuaji wa watotona changamoto zinazowakabili pamoja na vijana balehe, anakuwana uwezo mkubwa wa kutengeneza maudhui yenye manufaa kwa jamii.
Kupitia mafunzo haya, tumesisitiza umuhimu wa kuandaa vipindivinavyolinda maslahi ya mtoto, vinavyotoa elimu sahihi na vinavyochochea mawasiliano mazuri ndani ya familia”. Amesema SabrinaMwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la KuhudumiaWatoto (UNICEF) Alice Mwiru ambayeni Mtaalamu wa mabadiliko ya tabia za jamii, amehimiza waandishi wa habari kuongeza ubunifu na uwajibikaji katika utayarishaji wa vipindi vya Watoto, amesisitiza kuwa UNICEF itaendelea kushirikiana naSerikali kuboresha maudhui yanayohusu watoto ili kuhakikisha haki za mtoto na masuala yao yanapewa kipaumbele katika majukwaa ya habari.
Naye mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo Godliver Thomasi kutoka Jamii Forums amesema mafunzo hayo yamempa mwanga zaidi namna ya kuandaa vipindi husika.
“Mafunzo haya yamenipa uelewa mpana kuhusu namna ya kuandaa maudhui
yanayowagusa watoto na vijana kwa njia sahihi na yenye kujenga. Nimejifunza umuhimu wa kutumia lugha rafiki, kuzingatia hatua za
ukuaji wa mtoto pamoja na kuandaa vipindi vinavyofundisha na kuburudisha kwa wakati mmoja. Kupitia elimu hii, ninaamini nitakuwa sehemu ya kuleta mabadiliko chanya katika jamii kupitia kazi yangu ya uandishi wa habari”.

