Na. Fullshangwe Blog,Dodoma
Mkurugenzi Mkuu wa TMDA Dkt.Adam M. Fimbo ameongoza maandamano ya watumishi wa TMDA mkoani Dodoma katika kusherehekea sikukuu ya wafanyakazi duniani maarufu kama MEI MOSI yanayofanyika kimkoa katika viwanja vya Jamhuri.

Maadhimisho haya hufanyika kila mwaka tarehe 1 Mei, kila mwaka kwa ajili ya kuboresha mahusiano na kuweka mazingira bora mahala pa kazi.
Kwa mwaka huu maonesho haya yana kauli mbiu inayosema “Kazi zenye staha ni nguzo Imara kwa maendeleo Endelevu katika utekelezaji wa Dira ya Taifa 2050” ambapo kitaifa yanafanyika mkoani Njombe.

( Picha na Fullshangwe Blog )
