Mkuu wa wilaya ya Arusha,Joseph Mkude akifunga mafunzo hayo jijini Arusha
Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Arusha, Mhandisi Reginald Masawe akizungumza kwenye mkutano huo jijini Arusha
Happy Lazaro,Arusha .
Arusha .Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Joseph Mkude, amesema kuwa ,ajali za barabarani zinasababishwa na sababu mbalimbali, lakini usanifu duni wa barabara umeendelea kuwa miongoni mwa changamoto kubwa zinazohitaji ufumbuzi wa haraka.
Mkude ameyasema hayo leo jijini Arusha wakati wa kufunga mafunzo ya usalama barabarani jijini Arusha .
“Serikali imesisitiza umuhimu wa kuimarisha usanifu wa barabara kama njia madhubuti ya kudhibiti ajali na kulinda maisha ya wananchi, ikibainisha kuwa maboresho ya kitaalamu katika miundombinu yameanza kuleta matokeo chanya katika maeneo mbalimbali nchini.”amesema Mkude.
Amesema kuwa mafunzo hayo yameweka mkazo katika kuboresha usanifu wa barabara kwa kuzingatia viwango vya kitaalamu, huku yakitoa mifano halisi ya maeneo yaliyokuwa na ajali nyingi lakini sasa yamepata nafuu baada ya kufanyiwa marekebisho.
“Mfano ni barabara ya Bagamoyo-Tanga ambayo awali ilikuwa nyembamba na yenye kona hatarishi, hali iliyochangia ajali za mara kwa mara. Pia daraja la Mahandelea lilikuwa na changamoto kubwa kabla ya kufanyiwa maboresho,” alisema Mkude.
Naye Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Arusha, Mhandisi Reginald Masawe, amesema pamoja na juhudi za serikali kuboresha miundombinu ya barabara, bado matumizi yasiyo sahihi ya barabara yanaendelea kuhatarisha usalama wa watumiaji.
Ametaja baadhi ya changamoto kuwa ni pamoja na wananchi kufanya biashara pembezoni mwa barabara kuu, hali inayoongeza hatari ya ajali na kuhatarisha maisha.
“Usalama barabarani si jukumu la taasisi moja pekee, bali ni la kila mtumiaji wa barabara kuhakikisha anazingatia sheria na taratibu zilizowekwa,” amesema Masawe.
Aidha, amesisitiza umuhimu wa ushirikishwaji wa wadau katika hatua zote za miradi ya barabara ili kupata maoni ya wananchi na kupanga matumizi sahihi ya maeneo yanayozunguka barabara, hatua inayosaidia kupunguza ajali.
Amefafanua kuwa ajali za barabarani zina athari kubwa kwa taifa, ikiwa ni pamoja na kupoteza nguvu kazi, kuongezeka kwa gharama za matibabu, uharibifu wa vyombo vya usafiri pamoja na madhara ya kijamii kwa familia za waathirika.
Masawe ameongeza kuwa TANROADS imeanza kuimarisha mchakato wa usanifu kwa kushirikisha wataalamu wa usalama barabarani tangu hatua za awali za miradi, ili kubaini na kurekebisha maeneo hatarishi kabla ya ujenzi kuanza.
“Tunataka kuhakikisha kila mradi wa barabara unazingatia viwango vya usalama tangu usanifu hadi utekelezaji,” amesema .
Viongozi hao pia walisisitiza umuhimu wa kuendeleza mafunzo ya usalama barabarani kwa wadau mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari, wapangaji miji, Jeshi la Polisi na wataalamu wa miundombinu, ili kuongeza.




