Pembezoni mwa Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 40 ya Utawala wa Mfalme Mswati III, mjini Ezulwini, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, anayeshughulikia masuala ya Afrika Madhariki, Mhe. James Millya, amewasilisha salamu za pongezi kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Mfalme Mswati III wa Ufalme wa Eswatini.
Akipokea salamu hizo, Mfalme Mswati III amemshukuru Mhe. Dkt. Samia kwa salamu za pongezi na kueleza kuwa kitendo cha kutuma mwakilishi wake kwenye maadhimisho hayo ni ishara thabiti ya uhusiano mzuri na udugu uliopo kati nchi zote mbili.




