Rais wa Taasisi ya Wanaume Tanzania (Men at work Global) Maxwell Shing’oma akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) Jijini Mwanza
………
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Kongamano la wanaume (wanaume summit 2026) lenye lengo la kusaidia kuongeza hamasa ya wanaume kujitambua,kujifahamu na kujua wajibu na majukumu yao makubwa wanayoyabeba kwaajili ya jamii,familia na taifa kwa ujumla litafanyika kesho Jumapili Aprili 26, 2026.
Kongamano hilo limeandaliwa na taasisi ya Wanaume Tanzania (Men at Work Global) na litafanyika katika ukumbi wa Chuo cha Benkii Kuu (BoT) Jijini Mwanza.
Akizungumza leo Jumamosi Aprili 25,2026 na waandishi wa habari mkoani mwanza, rais na mwanzilishi wa Taasisi ya Men at Work Global, Maxwell Shing’oma amesema taasisi hiyo imesajiliwa mahususi kwaajili ya shughuli za wanaume ambapo siku hiyo ya kesho wanasherehekea miaka 11 tangu kuanzishwa kwake.
Amesema msingi wa uwanaume umejengwa katika malezi hivyo ukipotea kwenye malezi unakuwa umepotea jumla kwenye aina ya mwanaume unayemtaka.
“Siku ya kesho tukakuwa na ratiba mbili tutaanza na vijana wadogo kuanzia miaka 12 hadi 19 kwaajili ya kuwapa elimu ya masuala mbalimbali ikiwemo kupata fursa ya kujielewa mapema sanjari na kuwaandaa kuwa wanaume bora, baada ya hapo inaingia ratiba ya wanaume”,Amesema Shing’oma.
Aidha, amesema kuwa ushirikiano kati ya Serikali na taasisi hiyo ni mkubwa katika kuhakikisha wanawasaidia kuwapa vibali kwaajili ya kuingia kwenye shule kuzungumza na watoto wakiume,kuendesha mikutano kwa lengo la kutoa elimu.
“Pamoja na ushirikiano huo tunaiomba serikali iongeze nguvu zaidi ikiwemo kuwezesha fedha ili tuweze kuwafikia watu wengi zaidi”,




