Na. Sixmund Begashe, Njombe
Timu za Mpira wa Miguu Wanaume na Mpira wa Pete za Wizara ya Maliasili na Utalii zimeibuka na ushindi mnono dhidi ya timu za Ardhi na RAS Njombe katika michuano ya Mei Mosi 2026 inayoendelea Mkoani Njombe.
Katika Mchezo wa Mpira wa Pete Wanawake, Timu ya Maliasi imeibuka na ushindi mnono wa magili 34 -13 dhidi ya majirani yao timu ya Wizara ya Ardhi hali iliyo wajaza furaha washabiki wake waliojitokeza kuishangilia.
Akizungumzia mchezo huo Kocha Msaidizi wa timu ya mpira wa Pete Maliasili, Bi. Maimuna Kitete amesema huo ni mwanzo tu wa safari yao ya kuibuka na Kombe la mchezo huo.
Naye Naodha Msaidi wa timu ya Mpira wa Pete Ardhi Bi Siri Mrisho licha ya kuipongeza timu ya Maliasili kwa ushindi amesema wachezaji wake bado wako imara hivyo wawanauhakika wa kushinda kwenye michezo mingine iliyo mbele yao.
Aidha, mtanange katika ya timu ya mpira wa miguu Maliasili Wanaume na timu ya Mkoa wa Njombe, Maliasili imeshinda goli 4-0.





