Na Miza Kona, Maelezo Zanzibar
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendelea kuchukua hatua madhubuti kuhakikisha kuwa taasisi za viwango zinawezeshwa ipasavyo ili ziweze kusimamia ubora wa bidhaa na utoaji huduma.
Akizunguza katika Maadhimisho ya Siku ya Viwango Afrika huko Uwanja wa Mao Zedong kwa niaba ya Kaumu Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Mhe. Hamza Hassan Juma, Mkurugenzi Mkuu Wakala wa Vipimo Zanzibar (ZAWEMA) Mohamed Mwalim Simai, amesema nchi haiwezi kufanikiwa bila ya kuzingatia ubora kwani viwango husaidia kuondoa vikwazo visivyo vya lazima katika biashara, hujenga Imani kwa walaji na kuchochea ubunifu katika uzalishaji na utoaji wa huduma.
Amesema kuwa bidhaa zisizo na ubora zinaweza kusababisha madhara makubwa kwa jamii hivyo usimamizi madhubuti wa viwango ni jukumu la pamoja kati ya Serikali, sekta binafsi na wananchi kwa ujmla.
Aidha ameeleza kuwa Serikali itaendelea kuhamasisha sekta binafsi, wazalishaji wadogo na wa kati, pamoja na wafanyabiashara kuzingatia matumizi ya viwango katika shughuli zao za kila ili kuzalisha bidhaa zenye viwango nchini.
“Serikali ya awamu ya nanne ya Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi inatambua mchango wa Taasisi ya hizi za Viwango Afrika na itaendelea kuchukua hatua madhubuti za kusimamia na kuimarisha Taasisi ya Viwango ikiwa ni pamoja na kuimarisha mfumo ya viwangona ubora, kuhamasisha matumizi ya viwango vinavyokubalika kimataifa, kusaidia wafanyabiashara hasa MSMEs kufikia masoko mapana pamoja na kukuza mazingira ya biashara yenye haki na usawa”, ameeleza Kaimu huyo.
Kwa upande wa biashara kikanda Kaimu huyo amefahamisha kuwa viwango huchangia kwa kiasi kikubwa katika kurahisisha biashara baina ya nchi za Afrika kwa kupata viwango vinavyofanana au kutambulika kwa pamoja, kurahisisha usafirishaji na kuongeza ushindani wa bidhaa katika soko la Afrika na duniani.
Aidha amewasisitiza wafanyabiashara wadogo na wa kati kuzalisha bidhaa zenye kukidhi viwango ili kuepuka kuongeza kwa gharama, kupunguza ushindani kwa ajili ya kupata viwango vinavyofanana.
Kaimu Mohamed amefahamisha kupitia utekelezaji wa viwango vinavyolingana Afrika inaweza kutoka hali ya masoko yaliyogawanyika na kuingia katika mfumo mmoja wa uchumi uliounganishwa ambao unaokuza usawa, ustawi wa kiuchumi na ushindani katika soko la kimataifa.
Aidha ameipongeza Taasisis ya Viwango Zanzibar (ZBS) kwa juhudi zake kubwa katika kusimamia viwango, kukuza uchumi, kuelemisha jamii na kuiweka Zanzibar katika ushindani wa kimataifa katika uzalishaji wa bidhaa bora.
Hata hivyo amewataka wadau wote kushiirikiana kwa karibu katika kuimarisha matumizi ya viwango kwa kuzingatia ubora wa bidhaa zinazoidhinishwa, walaji wapate uelewa wa haki na usalama ya biadhaa ili kujenga uchumi imara kwa maslahi ya taifa.
“Naomba tuendelee kushirikiana ili kuhakikisha kuwa viwango vinakuwa msingi wa maendeleo ya taifa letu na Bara la Afrika kwa ujumla”, amesisitiza
Nae Mkurugenzi wa Wakala wa Viwango Zanzibar Yussuf Ali amesema maadhimisho ya Siku ya Viwango Afrika hufanyika kila mwaka ambapo Jumuiya Umoja wa Viwango Afrika huungana na kuandaa mashindano ya insha kwa wanafunzi vyuo mbali mbali kwa kutoa mada kwa ajili ushindani.
Amesema jumla ya wanafunzi 115 kutoka vyuo mbalimbali nchini kwa ngazi ya cheti, stahahada na Shahada wameshriki katika mashindano ya insha ambapo wanafunzi watano wamefanikiwa kufaulu katika mashindano ya uandishi wa insha na kupewa zawadi mbali mbali.
Maadhimisho hayo yaliambatana matembezi, mazoezi ya viungo pamoja na utoaji wa zawadi kwa washiriki na wadau wa ZBS.

