Meneja wa Kampuni ya Emichem Enterprises, Boniface Paulo.
………..
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Kampuni ya Emichem Enterprises iliyoko Mabatini Jijini Mwanza inatarajia kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa watu 2000 katika mwaka huu kwa lengo la kuwawezesha vijana,wakinamama na wakinababa kujiajiri wenyewe.
Mafunzo hayo ni pamoja na kutengeneza sabuni za maji,sabuni za miche shampoo pamoja na batiki ambapo wanapata elimu hiyo muhimu bure.
Akizungumza na Fullshangwe Blog Meneja wa Kampuni hiyo, Boniface Paulo amesema wao ni wabunifu wa vyanzo vya ajira kupitia uzalishaji wa bidhaa ambapo ameeleza kuwa dhamira yao ni kuona kundi la vijana linapata ajira kwakujiajiri wao wenyewe.
“Sisi Emichem Enterprise tunatoa elimu kwa wajasiriamali ili waweze kuwa na uwezo wa kutengeneza sabuni na bidhaa mbalimbali ambazo zitauzwa kwenye masoko yetu ya hapa ndani”,
Amesema kwa mwaka huwa wanatoa mafunzo kwa awamu nne na hadi sasa kwa awamu ya kwanza wameshafundisha vijana 97,wakinamama 121 na wakinababa 32.
Aidha, ametoa wito hususani kwa vijana kuchangamkia fursa ya mafunzo ili waweze kupata elimu itakayowasadia kujiajiri wenyewe