Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiwasili katika eneo la Bwawa la Mindu, ambacho ni chanzo kikuu cha Maji Safi kwa Manispaa ya Morogoro, kwa lengo la kukagua eneo hilo, ikiwa ni kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Maji 2026, inayofanyika mkoani Morogoro. Tarehe 22 Machi 2026.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akibonyeza kitufe kuzindua Mfumo wa Utabiri wa Kiasi cha Maji kwenye Mito Tanzania, wakati alipotembelea na kukagua Bwawa la Mindu, ambacho ni chanzo kikuu cha Maji Safi kwa Manispaa ya Morogoro, ikiwa ni kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Maji 2026, inayofanyika mkoani Morogoro. Tarehe 22 Machi 2026.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akipanda mti aina ya Mkarafuu, pembezoni mwa Bwawa la Mindu, ambacho ni chanzo kikuu cha Maji Safi kwa Manispaa ya Morogoro, ikiwa ni kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Maji 2026, inayofanyika mkoani Morogoro. Tarehe 22 Machi 2026.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akisikiliza maelezo kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Mwajuma Waziri, kuhusu Mpango wa Gridi ya Taifa ya Maji, wakati alipowasili katika Viwanja vya Mkwawa mkoani Morogoro katika Maadhimisho ya Kilele cha Wiki ya Maji 2026. Tarehe 22 Machi 2026.