Leo Machi 19, 2026 ujumbe kutoka Wizara ya Madini Makao Makuu ukiongozwa Mkurugenzi wa Sera na Mipango Augustino Olal umetembelea Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC) katika duka la Kituo hicho lililopo Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC.) jijini Arusha.
Ziara hiyo imekuwa na mazungumzo yenye tija kuhusu namna ya kukuza Sekta ya Uongezaji thamani madini nchini hususan kwa madini ya vito Tanzania ikiwemo kuimarisha uelewa wa wageni na wazawa juu ya vito vya thamani pamoja na bidhaa zinazotengenezwa kutokana na madini yanayopatikana nchini.
“Tunaamini kupitia ushirikiano huu, tunaendelea kuinua ubora, thamani na hadhi ya madini ya Tanzania kimataifa,”
amesema Mratibu wa TGC, Ally Maganga.

