Kadhalika Sheikh Mtupa ameipongeza TRA Mkoa wa Pwani kwa kuweka mikakati madhubuti ambayo imeweza kusaidia kwa kiassi kikubwa katika suala zima la kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato ambayo yanapelekea kuleta mabadiliko makubwa katika maendeleo kwa wananchi.
Kwa upande wake Meneja wa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Pwani Masawa Masawa amesema kwamba wameamua kufanya tukio la Iftar hiiyo na kuwakutanisha makundi mbali mbali ikiwa ni moja ya kurudisha fadhila kwa jamii pamoja na kukutana na watoto yatima na kula nao chakula cha jioni.
Meneja huyo amesema kwamba lengo kubwa la TRA Mkoa wa Pwani ni kuendelea kushirikiana begaa kwa bega na jamii katika mambo mbali mbali ikiwemo kukutana kwa pamoja na kubadilishanaa mawazo pamoja naa kula cha jioni kwani ni moja ya kuongeza wigo mpana ya katika kujenga mahusiano mazuri kwa jamii.

