Mkurugenzi wa biashara kutoka Azania benki ,Yahaya Mbanka akizungumza kwenye uzinduzi huo jijini Arusha leo.

Mkurugenzi wa kituo cha kimataifa cha mikutano cha AICC kilichopo mjini hapa,Christina Mwakatobe akizungumzia uzinduzi huo.

……….
Na Happy Lazaro, Arusha
Benki ya Azania yaendelea kusogeza huduma zake karibu na wananchi ambapo leo imezindua mashine ya ATM katika kituo cha kimataifa cha mikutano cha AICC kilichopo jijini Arusha .
Mkurugenzi wa biashara kutoka Azania benki ,Yahaya Mbanka amesema kuwa uwepo wa mashine hiyo utawasaidia wageni kupata huduma kwa urahisi wanapokuwa kwenye mikutano jijini Arusha.
Mbanka amesema kuwa,mashine hiyo ni ya kisasa kabisa ambapo kama una kadi ya viza ya benki yoyote unapotoka duniani unaweza kupata fedha kwa urahisi kupitia benki hiyo.
Naye Mkurugenzi wa kituo cha kimataifa cha mikutano cha AICC kilichopo mjini hapa,Christina Mwakatobe amepongeza uwepo wa benki hiyo kusogeza huduma karibu na wananchi hasa katika kituo hicho ambacho hutumiwa na watu kutoka mataifa mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.
Amesema kuwa,amefurahishwa sana na kitendo hicho kwani mara nyingi kuna mikutano ya watu kutoka maeneo mbalimbali ambapo wamekuwa wakipata changamoto katika kuhakikisha wageni wanaofika hapo wanaweza kupata huduma za fedha za kitanzania kirahisi .
“tuna furaha kubwa sana kuwakaribisha benki ya Azania kuwa sehemu ya Aicc kama mnavyofahamu tumekuwa tukipokea mikutano mikubwa ya kimataifa ndani na nje ya nchi ambapo kwa sasa wataweza kupata huduma za kutoa fedha kwa urahisi na kuweza kutimiza majukumu yao kwa haraka nawapongeza sana kwa kujiongeza.”amesema Mwakatobe.
Amefafanua kuwa, Benki hiyo imeleta chachu kubwa sana katika kituo hicho kwani tayari wageni wameshaanza kunufaika na uwepo wa benki hiyo katika eneo hilo.
