Meneja wa TARURA mkoa wa Arusha,Injinia Nicholas Francis akizungumza kwenye kikao hicho jijini Arusha.

Happy Lazaro,Arusha .

Arusha . TARURA Mkoa wa Arusha kwa mwaka wa fedha 2026/2027 imependekeza jumla ya Tsh Bilioni 19, 303, 251, 413.8 kwa ajili ya matengenezo ya barabara na madaraja.

Hayo yamesemwa leo jijini Arusha na Meneja wa TARURA mkoa wa Arusha,Injinia Nicholas Francis wakati akizungumza kwenye kikao cha kwanza cha bodi ya barabara kilichofanyika jijini Arusha .

Injinia Francis amesema kuwa, TARURA mkoa wa Arusha unahudumia mtandao wa barabara wenye jumla ya km 5752.834, madaraja 107 na makaravati 2639 kwa wilaya zote sita.

Aidha Injinia Francis amebainisha changamoto zinazowakabili kuwa ni pamoja na msongamano hasa maeneo ya katikati ya Jiji (CBD), uharibifu wa miundmiundombinu.

Hata hivyo ametaja changamoto nyingine kuwa ni pamoja na wizi wa alama za barabarani, kingo za madaraja, kutupa taka katika mifereji ya maji na barabara na kukata barabara bila kufuata utaratibu.“Changamoto zingine ni kilimo ama matumizi mabaya ya hifadhi za barabara kinyume cha sheria na kupitisha mifugo barabarani kinyume cha sheria ya barabara ya mwaka 2007 Na. 13 ya 2007 na kanuni zake za 2009.”amesema Injinia Francis .

“Katika mtandao huu wa km 5752.47 kati ya hizo barabara za lami km 170.407 (2.96%), barabara za changarawe km 1591.267 (27.66%) na barabara za udongo km3991.160 (69.38%)” aamefafanua Injinia Francis